Search form

2 TIM. int

UTANGULIZI

Kuhusu huyu Timotheo tazama utangulizi kwa Waraka wa Kwanaza kwa Timotheo. Inaaminika kuwa baada ya Paulo kuandika Waraka wa kwanza kwa Timotheo alitembelea baadhi ya Makanisa (2 Tim 4:13, 20) ndipo aliposhikwa akafungwa na baadaye akapelekwa Rumi tena akiwa mfungwa. Akiwa kule Rumi aliandika Waraka huu wa Pili kwa Timotheo (1:18; 2:9).

Tofauti na Nyaraka nyingine zote za Paulo, Waraka huu karibu wote unamlenga Timotheo binafsi. Hata hivyo, kama zile Nyaraka za kichungaji, huu nao unawahusu pia viongozi wa kanisa la kikristo. Mafundisho yake yanafaa sana kwa hao viongozi katika kuendelea kuishi vilivyo hapa duniani. Timotheo anaonekana katika Waraka huu kama mtu mwenye madaraka juu ya jumuiya kadhaa za kanisa na anashauriwa awatie moyo na kuwakinga na mitindo yenye kuangamiza imani ya kikristo kutoka nje na ndani. Anatakiwa kukiweka motomoto kipaji cha Mungu kilicho ndani yake (1:3-7), asiwe na haya kumshuhudia Kristo Bwana (1:8-18) na kushiriki sehemu yake ya mateso kama askari hodari wa Kristo (2:1-13).

Swahili Union Version

Swahili Union Version (SUV): Copyright - 1952, 1997: Bible Society of Tanzania and Bible Society of Kenya. All rights reserved.

Swahili Union Version (SUV): Hakimiliki -1952, 1997: kwa: Chama cha Biblia cha Tanzania na Chama cha Biblia cha Kenya. Haki zote zimehifadhiwa.

More Info | Version Index