Search form

ZAB. 41

Hakikisho la Msaada wa Mungu na Ombi la Uponyaji

Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi.

1-Heri amkumbukaye mnyonge;

BWANA atamwokoa siku ya taabu.

2BWANA atamlinda na kumhifadhi hai,

Naye atafanikiwa katika nchi;

Wala usimtie katika hali wamtakiayo adui zake.

3BWANA atamtegemeza alipo mgonjwa kitandani.

Katika ugonjwa wake umemtandikia.

4-Nami nalisema, BWANA, unifadhili,

Uniponye roho yangu maana nimekutenda dhambi.

5Adui zangu wananitaja kwa maneno mabaya,

Atakufa lini, jina lake likapotea?

6-Na mmoja wao akija kunitazama asema uongo,

Moyo wake hujikusanyia maovu,

Naye atokapo nje huyanena.

7Wote wanaonichukia wananinong’ona,

Wananiwazia mabaya.

8Neno la kisirani limemgandama,

Na iwapo amelala hatasimama tena.

9-Msiri wangu tena niliyemtumaini,

Aliyekula chakula changu,

Ameniinulia kisigino chake.

10Lakini Wewe, BWANA, unifadhili,

Uniinue nipate kuwalipa.

11Kwa neno hili nimejua ya kuwa wapendezwa nami,

Kwa kuwa adui yangu hasimangi kwa kunishinda.

12-Nami katika ukamilifu wangu umenitegemeza,

Umeniweka mbele za uso wako milele.

* * *

13-Na atukuzwe BWANA, Mungu wa Israeli,

Tangu milele hata milele. Amina na Amina.

Swahili Union Version

Swahili Union Version (SUV): Copyright - 1952, 1997: Bible Society of Tanzania and Bible Society of Kenya. All rights reserved.

Swahili Union Version (SUV): Hakimiliki -1952, 1997: kwa: Chama cha Biblia cha Tanzania na Chama cha Biblia cha Kenya. Haki zote zimehifadhiwa.

More Info | Version Index